TATIZO LA KUTOPATA UJAUZITO KWA MWANAMKE NA SULUHISHO LAKE.

JINSI YA KUTIBU TATIZO LA KUTOPATA UJAUZITO

TATIZO LA KUTOPATA UJAUZITO

 Kitaalamu linaitwa ‘Infertility’.
Hili ni tatizo ambalo limekuwa kubwa sana kwasasa, tatizo hili lipo kwa mwanaume na mwanamke, lakini leo tutalitazama zaidi  kwa upande wa mwanamke.
 Uchunguzi wa kutopata ujauzito kwa mwanamke hufanyika katika hospitali kwa madaktari wa akina mama. Vipimo vipo kwa mwanaume na mwanamke na vinakuwa tofauti.

Tunaposema ugumba ni kwamba watu wawili mke na mume kushindwa kupata mtoto kwa zaidi ya mwaka mzima bila mafanikio.

MATATIZO KWA MWANAMKE


Tatizo la kutoshika mimba kwa mwanamke husababishwa na sababu mbalimbali, Sababu hizo zimegawanyika katika makundi matatu.

1: Sababu za kurithi (Genetic factor)
Hii huhusisha zaidi kuwepo kwa   sababu za kurithishwa kwa tatizo hili katika familia.

2: Matumizi ya Dose au Dawa zinazozuia mimba/kutoa mimba / Dawa zinazoathiri mfumo wa uzazi kwa mwanamke.
Huhusisha zaidi matumizi ya madawa mbalimbali ambayo huwa yanajikita zaidi katika kutoa au kuzuia mimba kwa mwanamke hivyo kuathiri mfumo wa homoni kwa mwanamke.

3: Mfumo mbaya wa maisha
Ambao hupelekea kwa kuvurugika kwa homoni yaani hormonal imbalance,  vimbe za uzazi.

Mwanamke mwenye tatizo la kutoshika mimba anaweza kuwa na matatizo kwenye mfumo wa homoni kiasi kwamba mayai hayazalishwi au hayapevuki.
Pia mzunguko wa hedhi kuvurugika na matiti kutoa maziwa wakati hana mimba wala hanyonyeshi.

      Tatizo la kutopata ujauzito pia linaweza kusababishwa na maambukizi sugu katika viungo vya uzazi kunakosababishwa na magonjwa ya zinaa na  kuharibika mimba mara kwa mara. Tatizo hili la kuharibika kwa mimba kunaweza kusababishwa na aidha mimba kuharibika kwa bahati mbaya au kwa makusudi tatizo hili kwa  mwanamke huambatana na dalili mbalimbali kama vile:

kuumwa na tumbo chini ya kitovu kwa muda mrefu au mara kwa mara.
Maumivu haya ya chini ya tumbo yanaweza kuwa katikati au kuelekea kushoto au kulia chini ya tumbo.
Wakati mwingine mwanamke hulalamika maumivu makali wakati wa hedhi
 Maumivu wakati wa tendo la ndoa Na kutokwa na uchafu ukeni unaoambatana na muwasho.

Lakini pia Mwanamke mwenye matatizo haya hulalamika kutokupata ute wa uzazi unaoashiria upevukaji wa mayai.
 Kuvurugika kwa mzunguko na hajui mzunguko wake unavyokwenda,
 Pia hupoteza hamu na raha wakati wa tendo la ndoa.

Uchunguzi wa tatizo hili ni vipimo mbalimbali kama vipimo vya Ultrasound, vipimo vya damu kuangalia maambukizi na mfumo wa homoni au vichocheo vya uzazi, vipimo vya ukeni kuangalia kama kuna tatizo gani linaloathiri uzazi au maambukizi.
Mwanamke pia atafanyiwa vipimo vya mirija kuangalia endapo kama mirija ya uzazi imeziba au ina tatizo lolote.

Matatizo ya mirija ya uzazi ni kama vile kuziba mirija kutokana na athari za maambukizi au makovu ya ndani kutokana na upasuaji wa mirija au kizazi katika kuondoa uvimbe.
Maambukizi kama ‘PID’ na makovu husababisha viungo vya uzazi na vingine katika sehemu ya nyonga kushikamana.

  •  Maambukizi ya mirija husababisha mirija kujaa maji au mirija kujaa usaha hivyo kutopata ujauzito.

Dalili kuu ya matatizo haya ni maambukizi sugu chini ya tumbo.

JINSI YA KUONDOKANA NALO:

Uondokanaji  wa matatizo ya uzazi kwa mwanamke hutegemea na uchunguzi, mfano kama ni maambukizi, basi program ya  antibayotiki itatolewa kadiri  itakavyofaa.
 Matatizo katika mfumo wa homoni pia yana program yake kulingana na kiwango cha upungufu huo wa homoni.

Uzibaji wa mirija pia una njia zake za kuzibua kutegemea na uzibaji.
Uwepo wa uvimbe ndani ya kizazi na kwenye vifuko vya mayai pia ni tatizo kubwa ambalo suluhisho lake hutolewa kutegemea na jinsi ulipo na ulivyo na dalili zinazoambatana na uvimbe huo.

Matatizo ya uzazi kwa mwanamke ni tatizo kubwa linaloathiri mfumo mzima wa maisha ya mwanamke kimwili na kisaikolojia. Unashauriwa uwapo katika hali hii ni vyema kulipatia ufumbuzi mapema, kuzingatia lishe bora na pia kuepuka mazingira yasiyochangamani na watu kwa huchangia kuwa na msongo wa mawazo.

Mawasiliano:

+255716789967
+255755928588

Email: globalremedies255@gmail.com


Popular posts from this blog

TATIZO LA KUTOPATA UJAUZITO NA MVURUGIKO WA HOMONI KWA MWANAMKE - FEMALE INFERTILITY AND HORMONE IMBALANCE

TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NA CHANGAMOTO YA UZAZI KWA MWANAUME.

UGONJWA WA BAWASIRI [MIWASHO/MAUMIVU NA VIMBE SEHEMU YA HAJA KUBWA]